Ni siku ya furaha sana kwani kulikuwa na baraka za wageni toka madhehebu
mengine mbalimbali na wenyeji wao ambao ni WAADVENTISTA
WASABATO,vipindi hivi vilianza na changamoto ya uchache wa watu,lakini
ajabu kubwa,wanafunzi wa MUHIMBILI wakiwa ni jeshi kubwa walifika mara
baada vipindi kuanza.....
Vipindi vilianza kwa uimbaji,ambapo kama vile ilivyokuwa kawaida ya
kiumbe binadamu hupenda sana kusikiliza mziki,na hapa kulikuwa na
vikundi vingi na kwa huduma hii,watu walikuwa na shauku kuendelea tu na
kuimba mpaka lakini muda haukuwa rafiki mahali hapa..
|
the wave junior-brothers toka MUHIMBILI |
|
THE WAVE SENIOR BROTHERS TOKA MUHIMBILI |
|
KATIKATI NI GODFREY OTIENO NA WENZAKE WAKIIMBA |
|
baadhi ya wanakwaya ya IFM wakiimba |
|
washiriki wakifatilia kilekinachojili |
|
PICHANI:kulia ni mwenyekiti wa TUCASA-IFM na kushoto ni mwinjilisti BARAKA ambae pia ndie alikuwa mhubiri kwa siku hii... |
Baada ya kipindi cha uimbaji tulipata shuhuda kwa kazi hii
ilivyofanyika maeneo ya chuo ya IFM ni kwa wanafunzi na walimu pia...Kuliteuliwa
wawakilishi kuja kueleza kile kilichofanyika ambapo walieleza mambo yafuatayo juu ya kazi hii ya utume;
- Kazi
ya utume hii ilihitaji nguvu ya ROHO MTAKATIFU kwa walimu na
maprofesa wa dini kama waiskamu walikataa ujumbe hasa hawakupenda kusikia
jina YESU likitajwa mahala hapa..
Muda
pia nao ulikkuwa ni changamoto kwani vipindi huingiliana na kzi hii,wakati
kazi inaendelea pia kulikuwa na vipindi vinaendelea katika madarasa
kwa washiriki wa huduma hii.... Mwisho vipindi hivi
vilihitimishwa na taarifa fupi toka kwa MWENYEKITI wa TUCASA-IFM,hapa
alinza kwa kusema kuwa kazi hii ya uinjilisti wa kugawa vitabu na
vijizuu,ambapo kati ya vitabu vya TUMAINI KUU 92,vitabu 82
viligawawiwa na vijizuu kati ya maboxi na sasa vimebaki vya kushika
mkononi.
No comments: